MSCHERANO KUONGEZA MKATABA BARCELONA.

Javier Mascherano.
KIUNGO wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona ya Hispania Javier Mascherano anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Mascherano ambaye amekuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona toka alipotua hapo kwa ada ya paundi milioni 22 kutoka Liverpool mwaka 2010 ambaye alinunuliwa kuja kuziba pengo la Yaya Toure ambaye aliondoka. Ingawa katika msimu wa pili akiwa na klabu hiyo amekuwa akichezeshwa kama beki wa kati na anatarajiwa kuja kuongeza mkataba na klabu hiyo yenye maskani yake katika Uwanja wa Camp Nou pindi atakpomaliza likizo yake. Wakala wa mchezaji huyo Walter Tamer alikaririwa akisema kuwa wako katika makubaliano mazuri na Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo Andoni Zubizarreta katika mkutano wao waliofanya Mei mwaka huu. Kwa mujibu wa tetesi hizo Mascherano anatarajiwa kuongeza mkataba wa miaka miwili katika mkataba wake wa awali ambao unaishia 2014.