KIZA kinene kimetanda kwenye siku, tarehe au mwezi wa
kufungwa kwa ndoa ya msanii anayefanya vizuri kwenye gemu la sinema za Kibongo,
Rose Donatus Ndauka na mchumba wake, Malick Bandawe.
Akizungumza na safu hii hivi karibuni ndani ya ofisi ya
Ndauka Entertainment iliyopo Mwananyamala jijini Dar, Malick alisema hatima ya
ndoa yao ipo mikononi mwa wazazi wao ambao ndiyo wanaojua tarehe na mwezi wa
kufungwa.
“Mimi binafsi si msemaji wa familia yangu, lakini ukweli ni
kwamba wao ndiyo wanajua tarehe na mwezi na wakati utakapofika naamini watu
wote watajua,” alisema Malick.
Hata hivyo, mume huyo mtarajiwa alisema anachojua yeye ndoa hiyo itafungwa mwaka huu.
Hata hivyo, mume huyo mtarajiwa alisema anachojua yeye ndoa hiyo itafungwa mwaka huu.