Mmoja
wa wasanii mahiri katika fani ya uigizaji hapa nchini,Wema Sepetu
akifanya mahojiano mafupi na Millard Ayo wa Clouds FM mapema leo kwenye
amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta ambalo linafanyika jioni ya
leo mpaka lyamba ndani ya uwanja wa chuo cha Ushirika,ndani ya mji wa
Moshi,ambapo katika tamasha hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni nusu
mnyama tu a.k.a 5,000/= kwa kila kichwa.
Wema Sepetu pia akizungumzia ujio wao ndani ya mji wa Moshi,kuwa wao kama Wasanii Nyota wa Filamu wamewasili mkoani humo kusaka vipaji vipya mbalimbali vya filamu,usahili huo unafanyika kwenye ukumbi wa Mr Price,ulioko mtaa wa Malindi.
Mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo akiwa Live mapema leo mtaa wa Malindi katika mpango mzima wa amsha amsha kwa wakazi wa Moshi kuhusiana na tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ambapo pia katika tamasha hilo kutatolewa zawadi mbalimbali ikiwemo gari ndogo aina ya Vits kama uinavyo pichani ikinadiwa vilivyo.
Kawa kawa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta pia linatoa mafuta kwa magari daladala,pikipiki sambamba na baji lita 10 ama tano kutoka kampuni ya Gapco ambao pia ni sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo.
Msanii mwingine nyota katika tasnia ya filamu,Aunt Ezekiel akielezea ni namna tamasha la Serengeti Fiesta lilivyowambamba wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake,na pia ujio wao kuwatafuta wasanii wapya chipukizi katika tasnia hiyo ambayo imekuwa ikikua siku hadi siku.
Wema Sepetu katika pozi na washabiki wake mapema mchana huu.
Mastaa wetu wa filamu hapa nchini,wametokelezeaje sasaaa.
Kiongozi wa msafara wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Mully B akiwa na mastaa wa filamu,Wema Sepetu na Aunt Ezekiel afu fulllll BBM kama kawa.
Millard Ayo akifanya mahojiano na Ray a.k.a Vincent Kigosi kuhusiana na ujio wao ndani ya mji wa Moshi
Kutoka kushoto ni Mr Hatman,Steve Nyerere,Bonge pamoja na Millard Ayo katika shoo love ya pamoja.
Wema Sepetu akijiweka sawa.
Wakiwa katika mazungumzo yao ya hapa na pale.
Kila mmoja ana haki ya kupata habari na kuhabarishwa.
Pichani ni Gari aina ya Vits itakayotolewa jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,kwa mshindi atakaejishindia kwenye droo itakayofanyika katika uwanja wa chuo cha ushirika,ambako tamasha hilo litarindima mpaka majogoo.
Jacob Steven a.k.a Steven akifafanua jambo mapema leo mtaa wa Malindi kuhusiana na suala zima la wasanii hao kulivamia jiji la Moshi