Bibi Cheka apikika na Godzilla kwenye wimbo mpya


Kama ulikuwa unadhani Bibi Cheka amekuja kujaribu kwenye muziki wa kizazi kipya, basi ni muda wa kulifuta wazo hilo katika kichwa chako.

Bibi Cheka is there to stay! Na sasa, ladies and gentlemen kaa tayari kwa ngoma mpya kutoka kwa msanii huyu mwenye umri mkubwa kuliko wasanii wote wa Bongo Flevan aliyomshirikisha Mfalme wa Salasala Godzilla.
Wimbo huo jana ulikuwa katika hatua za kurekodiwa ambapo mpishi Zullesh ndiye aliyehusika katika kutengeneza ngoma hii ya pili ya Bibi Cheka.
Wimbo unaitwa ‘Good Brother Fella’ ambao kwa mujibu wa Godzilla, bibi kapiga swagga za nguvu na kuonesha kuwa pamoja na umri wake kuwa mkubwa ngoma ya vijana anaiweza.
Jina la wimbo linaashiria kuwa, Bibi Cheka anataka kutumia fursa hiyo kumshukuru Said Fella ambaye ndiye aliyemfikisha hapo alipo na kumtoa katika uuzaji wa vitumbua/mandazi.
Tusubiri tuone awamu hii bibi yetu anatokaje baada ya wimbo wake wa kwanza aliomshirikisha Temba kufanya vizuri.