Sehemu ya Wajumbe wa bodi ya barabara mkoa Singida
Singida,
Juni 04,2012.
SERIKALI imeagiza viongozi, watendaji na wataalamu kutoa elimu ya kutosha katika maeneo ambayo barabara ya lami imejengwa, ili kuepuka uharibifu wa alama za barabarani, unaofanywa na baadhi ya Wananchi wasiokuwa waaaminifu, kwa kuzing’oa kwa makusudi.
Amesema barabara ni chachu ya maendeleo ya jamii katika kukuza uchumi wao na nchi kwa ujumla, hivyo ni lazima zitunzwe ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.
“Wito wangu kwenu, tushirikiane kuwadhibiti watu hawa, mimi binafsi nilikwishaanza zoezi la kutoa elimu, Februari 2012 nilifanya mikutano katika vijiji vya Kititimo na Kinyamwenda…..Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Polisi, hii iwe ni sehemu ya kazi zenu,”alisisitiza Dk. Kone.
Baadhi ya wajumbe walilalamikia ung’oaji vyuma vilivyowekwa kwa ajili ya alama barabarani na kwenda kuuza kama vyuma chakavu, na kuomba jeshi la polisi kudhibiti hali hiyo.
Hata hivyo wajumbe wengine wametoa tahadhari ya biashara ya vyum, iliyoshamiri nchini, hali inayohatarisha usalama wa magari, ambayo hukatwa katwa vipande na kupakiwa kwenye Fusso kwa ajili ya kusafirishwa jijini Dar es Salaam, kuuzwa kama vyuma chakavu.
Na Elisante John