Msanii mahiri wa HIP HOP ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Mr II' a.k.a Sugu, juzi alizikonga nyoyo za mashabiki wake waliofurika ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa kufanya makamuzi ya hatari katika tamasha la Usiku wa Sugu. Sugu alisindikizwa na Juma Nature, Profesa Jay, Vinega, Mkoloni na wengineo wengi kwenye shoo hiyo iliyokuwa ya aina yake.
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari a.k.a (Dogojanja) nae akitoa 'verse' kuupamba usiku wa Sugu ndani ya Dar Live.
Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan akiwasalimia mashabiki wa Dar Live
Nyomi iliyohudhuria Usiku wa Sugu.
Na Abby Mrisho