MWENYEKITI
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita
amesema kama siyo busara za Rais Jakaya Kikwete kukiongoza chama hicho,
tayari kingekuwa kimesambaratika.
Pia,
Guninita ameonya kuwapo watu wanaotumia vibaya jina Rais Kikwete katika
uchaguzi wa CCM unaoendelea nchini. Akizungumza Dar es Salaam na
viongozi wa CCM Kata ya Mbezi Juu mwishoni mwa wiki iliyopita,Guninita
alisema kuwapo kwa chama hicho licha ya wengine kudai kuwa kimepoteza
mvuto na haiba mbele ya umma, kumetokana na busara za Rais Kikwete.
Guninita
alisema tangu Rais Kikwete ashike usukani wa chama hicho, kimepita
kwenye mawimbi makali ambayo kama siyo busara zake yalikuwa
yanakizamisha.
“Amekuwa
(Rais Kikwete) akitumia vikao kumaliza misuguano inayotokea kwa baadhi
ya wanachama… tangu ashike usukani wa chama mwaka 2006, CCM imekumbwa na
mawimbi mazito lakini busara zake zimeokoa jahazi kuzama,” alisema
Guninita.
Kuhusu
baadhi ya wanachama wanaopita pita wakitumia vibaya jina la Rais
Kikwete, Guninita aliwaonya kuacha mara moja kwa sababu ana uhakika
hakuna aliyetumwa zaidi ni kuchafua jina linalo heshimika kwa wananchi.
Alisema
hali hiyo imesababisha watu wengine wenye nia ya kugombea nafasi za
uongozi kuogopa kujitokeza kuchukua fomu na kuzua malalamiko.
“Ni
haki ya kila mwanachama na kila kiongozi kugombea,huyo anayesema
ametumwa na JKni mnafiki mpuuzeni,hata kwenye nafasi yangu jitokezeni
hiyo ndiyo demokrasia,”alisema Guninita.
Alisema
mtu anayetumia jina la viongozi wakubwa licha ya kuwatisha wanachama
wenzake, anakiharibu chama na kudhalilisha demokrasia. Pia,aliwataka
wanachama wa chama hicho kuchagua viongozi bora wanaopenda kushirikiana
na wenzao,ambao watakisaidia chama kushinde chaguzi mbalimbali.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz