Wananchi Isimani Waongea Na Mbunge Wao

Na  Francis Godwin Blog
WANANCHI wa jimbo la Isimani mkoani Iringa wamepongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na mbunge wao Wiliam Lukuvi na kumtaka mbunge huyo kuwawabana watendaji wasio wasio wajibika kwa wananchi.

Wananchi hao walitoa pongezi hizo leo kwenye ukumbi wa Hima Isimani wakati mdahalo wa wazi Kati ya mbunge Lukuvi na wananchi ,mdahalo ulioandaliwa na asasi za kiraia Tanzania na kuratibiwa na asasi ya ISICO mkoa wa Iringa.
Akizungunza kwa niaba ya wenzake Maneno Kalinga alisema kuwa mbunge Lukuvi ni mbunge pekee katika mkoa wa Iringa kwa kufanya kazi karibu na wananchi wake ikiwa ni pamoja na kushughulikia kero za wananchi wake .
Kwani walisema kuwa baadhi ya watendaji wa kata hiyo wamekuwa wakishinda mjini Mara zote na kuacha ofisi jambo ambalo limekuwa ni kero kubwa kwa wananchi .
Hivyo walimtaka mbunge Lukuvi kuwawezesha watendaji hao wa vijiji kupata semina ila kujua majukumu Yao badala ya kugeuka watalii katika ofisi hizo za vijiji.

Wakati Lucy Kaginga alieleze kusikitishwa na tabia ya walimu wa shule ya Msingi Kising'a Isimani kuwatumikisha watoto katika shuguli za kuchota maji kwa ajili ya kujenga nyumba ya mwalimu badala ya kusoma.
Kwani alisema kuwa tabia hiyo imekuwa ni kero kubwa kwa wanafunzi hao na wazazi wanaomba mbunge kukomesha hali hiyo.
Wakati huo huo mbunge Lukuvi amewataka wananchi wa jimbo hilo kuweka utaratibu wa kuchangia chakula katika shule za Msingi ili kusaidia kuboresha Elimu kwa wanafunzi wa shule za Msingi na kupunguza Utoro kwa wanafunzi.

Mbunge Lukuvi ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera ya uratibu wa bunge ametazama hayo katika mdahalo wa wazi uliofanyika katika ukumi wa Hima kata ya Isimani mdahalo Kati ya wapiga kura wake na mbunge huyo ,mdahalo ulioendeshwa na asasi isiyo ya kiserikali ya ISICO mkoani Iringa.
Akizungunza kwa niaba ya mbunge huyo katibu wake Thoma Malenga alisema kuwa kero ya wanafunzi kushinda na njaa ama kurudi nyumbani mchana kwa ajli ya kupata chakula cha mchana linaweza kutatuliwa iwapo wananchi watakuwa na mkakati wa kuchangia chakula kwa ajli ya watoto hao.

Kwani alisema kuwa ili kupunguza Utoro kwa. Wanafunzi hao lazima wananchi kuweka mkakati. Wa kuhamasishana kuanzisha mpango wa kuchangia chakula ili watoto hao kupata chakula wakiwa shule.

Kuhusu kero ya maji katika eneo Hilo la Isimani Alisema kuwa tayari mkakati wa kuwaunganisha wananchi hao na mradi wa maji wa uhakika unafanyika na wananchi wategemee kupata huduma hiyo ya maji .
Aidha aliwataka wananchi waliowekewa alama za x katika nyumba zao kwa ajili ya kupisha upanuzi wa barabara ya Iringa - Dodoma kujiandaa kulipwa fidia kupitia wakala wa barabara mkoa wa Iringa ( TANROADS)