CHUZ,ROSE WA CHUZ WAMWAGANA

HATIMAYE ule uchumba wenye makeke wa Mkurugenzi wa Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ na msanii wa kundi hilo, Rose Michael ‘Rose wa Chuz’ umekatika na wawili hao wamemwagana, Risasi Mchanganyiko lina ushahidi mkononi.



Rose Michael ‘Rose wa Chuz’.

Tuesday Kihangala ‘Chuz’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao wamemwagana kufuatia timbwili zito aliloliangusha Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ nyumbani kwa Chuz hivi karibuni akimtuhumu demu huyo kumtesa mwanaye wakati baba mtu alipokuwa Zanzibar ‘Zenji’ akirekodi filamu ya Dirty Game.
Habari zinasema baada ya Chuz kurejea kutoka Zenji, Rose alitoa dukuduku lake kwamba, hawezi kuendelea kulea ‘toto ambalo’ mama yake hana shukurani.
“Kisa cha hawa watu kumwangana ni Jini Kabula, Chuz alikwenda Zenji kushuti filamu, aliporudi akakuta Rose amevimba macho kwa kulia, alipoulizwa kasema Jini Kabula alimfanyai fujo akimtuhumu kumtessa mwanaye.
“Chuz alijaribu kumlainisha Rose kwa maneno ‘matamtam’ lakini hakukubali, akaondoka kurudi kwao Arusha, hivi leo (juzi, Jumatatu) ninavyoongea na wewe, Rose yupo Arusha kwa wazazi wake,” kilisema chanzo hicho.
Paparazi wetu alimsaka Chuz kwa simu ya kiganjani na alipopatikana na kusomewa mashitaka yake, alikuwa na haya ya kusema:
Chuz: Aaah! Kifupi ni kwamba, ‘asa hivi mi naangalia kazi bwana. Unajua filamu za Bongo zinauza sana, lakini hata hivyo, tumejitahidi kuwa kama Wanaijeria, si eti?”
Risasi Mchanganyiko: Jibu swali langu, ni kweli umemwagana na Rose?
Chuz: Rose yupo, unajua yule demu (Rose) atakuja kuwa staa mkubwa sana haba Bongo, mi nakwambia. Anajua kuuvaa uhusika katika filamu. Ha! Ha! Ha! Ha!
Rose alipopigiwa simu siku ya Jumatatu iliyopita hakuweza kupatikana mara moja hewani.
Mapema mwaka huu, moja ya magazeti ya Global Publishers liliripoti Chuz kutangaza hadharani kwamba Rose ni mchumba wake na wangefunga ndoa katikati ya mwaka huu. Aliongeza kuwa msichana huyo ndiye mwanamke wa maisha yake baada ya wote waliopita.
Hata hivyo, Gazeti la Amani likaja andika habari zilizotoka kinywani mwa Jina Kabula akimuasa Rose kuwa makini na Chuz kwamba katika wanaume waongo ulimwenguni, jamaa huyo anashika nafasi ya pili.
Mbali na Rose, Chuz ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Joan Mutovolwa, Leila Ismail ‘Lilly’ (amezaa naye) Miriam Jolwa Jini Kabula (amezaa naye).