HII NDO FAMILIA YA JOSE CHAMELEONE



Daniela akiwa na wanae Abba na Alfa nchini Italia
Jose Chameleone anaweza kuonekana jeuri na mtata mbele ya mashabiki wake. Lakini kuna kitu kimoja ambacho wengi wanaweza wasiwe wanafahamu.
 Chameleone ni baba anayeipenda familia yake na anayewajibika kuiweka katika mazingira mazuri kadri awezavyo.Chameleone ana watato wanne. Mtoto wa kwanza ambaye ni wa kike anaitwa Ayla Mayanja Onsea aliyemzaa kwenye mahusiano yake na Dorotia. 

Leo (September 18, 2012) msanii huyo kupitia ukurasa wake Facebook, ameweka picha ya Ayla anayeonekana kukua, huku akiandika ‘Guess’.
Ayla Mayanja, mtoto wa kwanza wa Jose Chameleone
Katika ndoa yake na Daniella, Chameleone ana watato watatu. Abba Marcas Mayanja akiwa wa kwanza kwenye ndoa yao, Alfa Mayanja mtoto wao wa pili na Alba Shyne Mayanja aliyezaliwa February mwaka huu.

Alba Marcas Mayanja

Alfa Mayanja na Abba
September 3 mwaka huu, himaker huyo wa Valu Valu, aliamua kuvishambulia vyombo vya habari vya nchini Uganda kwa kuandika habari za uongo juu ya familia yake, “it’s a pity how media is telling lies for money!! I am clearing the air,my beautiful wife, Abba, Alfa and Alba are not in Mutungo as alleged by media, my family is on holiday in Italy, and not bothered by the rubbish haters are trashing! Please respect peoples families, my family please enjoy your holiday!!!! No stress!”

Hivyo pamoja na kuonekana kama ni mzee wa shari, mashabiki wanatakiwa kujua kuwa Chameleone ‘is a responsible father’.