Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (kulia),
akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 10, Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa
Mamlaka ya Elimu nchini (TEA), Seif Mohammed.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akifungua
hafla hiyo. Wengine pichani ni Eric Shigongo (kulia) na Seif Mohammed
(katikati).
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (katikati) akisisitiza jambo katika hafla hiyo.
Seif Mohammed (kushoto), akiishukuru Global Publishers na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kuchangia mfuko huo.
Sehemu ya wanahabari waliokuwa kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wanahabari wakipata lunch.
Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd leo imetoa
hundi ya shilingi milioni 10 ikiwa ni sehemu ya mapato yaliyopatikana
kwenye Tamasha la Matumaini lililoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya
kuchangia ujenzi wa hosteli za wasichana nchini. Kampuni hiyo imetoa
hundi hiyo kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Atriums
iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam