CHAMA CHA WANANCHI CUF CHALALAMIKIA VYOMBO VYA USALAMA

Mwenyekiti wa Chama cha wananchi  CUF  Profesa Ibrahim Lipumpa(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam juu ya Ajali ya Kuzama kwa Meli ya MV Skagit ya Kampuni ya Seagul na Maafa ya Abiria  waliozama na Kufa Maji iliyotokea Tarehe 18/08/2012. Ambapo alitoa lawama kwa Vikosi vya ulinzi na kusema kuwa  vilikosa kutimiza  wajibu wao kwa wakati, kwa mfano kikosi cha KMKM kilifika katika eneo la tukio saa 12 jioni wakati kikosi cha wanamaji cha JWTZ kilifika katika eneo la tukio  siku ya pili yake jambo ambalo  ilisababisha  watu wengi kufa kwa kukosa msaada wa kuokolewa.

 Aidha alisema kuwa Chama kinawasiwasi na manahodha  na Mabaharia katika kujua uwezo wa chombo chao kama kina uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa  kwa siku husika. “Tunawasiwasi na manahodha pamoja na Mabaharia na Pengine hata SUMATRA na wakala wa meli Zanzibar  ZMA haina sifa sahihi za manahodha na Mabaharia hawa.kulia ni Naibu mkurugenzi  wa Mipango uchaguzi  na Bunge Sheweji Mketo na wakwanza kushoto ni Abdul Kambaga Naibu mkurugenzi wa Habari na uenezi.