HISPANIA HAIJAFIKIA UBORA WA KIKOSI CHA BRAZIL MWAKA 1970 - PELE
|
Pele. |
MCHEZAJI nyota wa zamani
wa Brazil, Pele amesema kuwa kikosi cha nchi hiyo ambacho kilinyakuwa
Kombe la Dunia mwaka 1970 kilikuwa na wachezaji wengi wenye vipaji
ukilinganisha na kikosi cha sasa cha Hispania ambacho kimefanikiwa
kutetea taji la michuano ya Ulaya. Akiulizwa
kuwa ni timu ingeshinda kati ya hiyo ya Brazil ya mwaka 1970 na
Hispania ya hivi sasa nyota huyo wa zamani alijibu kwa kujiamini kwamba
kama angekuwa anacheza isingekuwa na shaka kwamba wangeshinda mtanange
huo. Hispania
ambao wameshinda mataji mawili ya Ulaya mfululizo pamoja na lile la
Kombe la Dunia 2010 imekuwa timu ya kwanza katika historia kushinda
mataji matatu makubwa ya kimataifa. Ustadi
wa kumiliki mpira ulioonyshwa na wachezaji wa Hispania na kuwasadia
kutete taji lao hilo umefananishwa na ule wa kikosi cha Brazil cha mwaka
1970 ambacho kilikuwa na wachezaji kama Pele, Rivellino, Gerson, Tostao
na Jairzinho ambao walinyakuwa Kombe la Dunia nchini Mexico kwa
kuifunga Italia kwa mabao 4-1 katika mchezo wa fainali. Pele
alistaafu kucheza soka mwaka 1971 na hakuwepo katika kikosi cha Brazil
ambacho kilishiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1974 ambapo
kilimaliza katika nafasi ya nne.