Marehemu Steven Kanumba.
MAREHEMU Steven Kanumba amewaliza tena baadhi ya mastaa wa Bongo Movie walioenda jijini Tanga kwa ajili ya Tamasha la wazi la filamu, Tollywood Newz inakupa kisa kamili.
Kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyekuwepo eneo la tukio, mastaa hao walishindwa kuvumilia na kumwaga machozi jukwaani kwa ajili ya kumkumbuka staa huyo aliyetangulia mbele ya haki.
Chanzo cha kilio hicho kilichotokea katika Viwanja vya Tangamano ni baada ya mshehereshaji wa shughuli hiyo, Chiki Mchome alipowataka waalikwa, wasanii na mgeni ramsi kusimama kwa dakika moja kumkumbuka marehemu.
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake Sinza Vatican jijini Dar.