Link Prezzo atajwa kwaajili ya ‘Elimination’

Link

Mfalme wa Bling nchini Kenya, Prezzo huenda akayaaga mashindano ya Big Brother Africa wiki hii kama hatopata kura za kutosha kutoka kwa mashabiki wake kwakuwa ametajwa kwenye kikaango cha Elimination.Hii ni habari mbaya kwa rapper huyo ambaye hivi karibuni ametokea kuwa adui wa nchini zingine za Afrika, husasan Nigeria na Afrika kusini.
Mbaya zaidi licha ya kusaidiwa wiki mbili zilizopita na Goldie, Prezzo amemtaja Goldie kwaajili ya kutolewa kwenye shindano hilo kitu ambacho kimewafanya aonekane msaliti na watu wa Afrika Magharibi kujiunga na Afrika Kusini kuchukia na kuponda chochote anachofanya Prezzo.
Hata hivyo kila nchi itahusika na kumpigia kura mshiriki wake ambapo Lady May, Kyle, Prezzo, Goldie, Junia na Keagan wapo kwenye kikaango hicho wiki hii.
Hiyo ina maana kuwa wakenya ama hata watanzana na waganda wanatakiwa kupiga kura kwa wingi kumwokoa Prezzo.