Mashabiki
wa Simba, jana wamemtembezea kichapo mama mmoja aliyekuwa amevalia
jezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars yenye nembo ya
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), kosa kukaa kwenye jukwaa
walilokuwa wamekaa wao.
Sasa
haikuweza kufahamika mara moja, mashabiki wa Simba wana bifu na TFF au
hawapendi timu ya taifa. Mama huyo alikimbizwa huku akipewa kichapo
hadi kutokwa damu, kabla ya kuokolewa na Polisi waliomteremsha
jukwaani. Aliporwa vitu vyake kama pochi na kadhalika.
Baadaye
akiwa amekwishaokolewa na askari, ndipo msamaria mwema mmoja, albino
akamuokotea baadhi ya vitu na kuwakabidhi askari. Huwezi kulipa jina
lingine tukio lile, zaidi ya udhalilishaji wa kijinsia. Alikuwa anatia
huruma mama huyo wakati anahangaika kujitoa kwenye kundi la mashabiki
wa kiuma wa Simba, iliyofungwa 3-1 na Azam katika Robo Fainali ya
Kombe la Kagame.
Picha na Habari Kwa Hisani ya Bin Zubery wa BongoStaz.Blog