MFUNGO MTUKUFU WA RAMADHANI WAMTESA NISHA

MSANII kunako anga la sinema za Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameweka wazi kuwa yupo katika wakati mgumu kwani Mwezi Mtukufu wa Ramadhan umemtega kwa vile mapenzi yake na jamaa anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu ndiyo kwanza yameanza.Akijilipua kwa Mpekuzi Newz, Nisha alisema katika kipindi hiki cha swaumu analazimika kukaa mbali na mwanaume huyo kwa sababu si wanandoa.

“Huu ni mtihani jamani lakini sina jinsi, acha nifunge nisije nikaharibu swaumu yangu bure, ila nitamshauri tukimaliza mfungo anioe kabisa,” alisema Nisha.