BAADA
ya hivi karibuni msanii wa filamu Bongo, Tamrina Mohamed Poshi
‘Amanda’ kutukanwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa ni mgumba,
mwenyewe amefunguka na kusema madai hayo si ya kweli.Akiongea na mwandishi wetu , Amanda alikiri kutukanwa katika mtandao
kuwa yeye ni mgumba kwa vile alikaa kwenye ndoa kwa miaka minne bila
kuzaa.
“Mimi si mgumba, niliwahi kubeba mimba miaka ya nyuma ikatoka. Pia umri wangu bado mdogo kuitwa jina hilo, sikutaka kuzaa kwenye ile ndoa kwa sababu zangu,” alisema Amanda.