MKOSI KWA SIMBA: AMIR MAFTAH KUIKOSA KAGAME - AVUNJIKA

BEKI wa pembeni wa Simba, Amir Maftar ameondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo kinachoshiriki michuano ya kombe la Kagame inayoendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Maftar ameondolewa kwenye kikosi hicho baada ya kidole chake cha mkono wake wa kulia kuvunjika, kwenye mechi dhidi ya Ports iliyochezwa jana saa 10: 00 jioni iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 3-0.
Kwa mujibu wa Daktari Mkuu wa timu hiyo, Cosmas Kapinga amesema kufuatia majeraha hayo aliyopata amevishwa P.OP kutokana na maumivu aliyoyapata katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Daktari huyo amesema, huenda akizikosa mechi zote zinazofuata za michuano hiyo inayoendelea, timu ikifuzu hatua ya robo ya fainali kwa ushindi huo walioupata .

“Maftar tumemuondoa kwenye kikosini, baada ya kupata majeraha ya kidole chake cha mkono wake wa kulia kuvunjika na kusababisha avishwe P.O.P, aliumia katika mechi na Ports tuliyocheza jana,” alisema Kapinga