Jeshi
la Polisi mkoani Singida, limemefikia azimio hilo baada ya kumhoji
Mnyika kwa saa tatu juzi usiku, kuhusiana na tukio hilo la mauaji
lililotokea baada ya mkutano wake wa hadhara uliofanyika Julai 14 mwaka
huu, majira ya jioni.
Mahojiano
hayo yaliyoanza saa 11.53 jioni na kumalizika saa 3:15 usiku,
yaliendeshwa chini ya kikosi maalum cha askari wa upelelezi kutoka
jijini Dar es Salaam kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani hapa.
Habari
zilizolifikia gazeti hili jana zilithibitisha kwamba Jeshi la Polisi
lilimtaka Mnyika awe tayari kuitwa wakati wowote ili kusaidia kwenye
kesi hiyo ya mauaji.
Tayari
watu 18 wametiwa mbaroni, miongoni wakiwemo wanachama wa Chadema, kwa
tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya kijana huyo wa CCM.
Mnyika alihojiwa huku akiwa na wakili wa Chadema na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mauaji
hayo ya mwenyekiti wa UVCCM yalifanyika Julai 14 mwaka huu saa 10 jioni
huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba
magharibi.
Mauaji
hayo yanadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na vurugu zilizotokea
kwenye mkutano wa hadhara ambao Mnyika alikuwa mgeni rasmi.
Katika
hatua nyingine, mshauri na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Dk Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa ameambatana na Mnyika,
alitarajiwa pia kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo jana.
Chanzo: www.mwananchi.co.tz