Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu alitembelea Msitu wa
Hifadhi ya Kazimzumbwi ulioko wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kujionea
uharibifu wa mazingira unaofanywa na kikundi cha watu wanaotaka
kujitwalia maeneo ndani ya msitu kuanzisha makazi yao.
akizungumza
baada ya kujionea uharibifu huo na kukagua mipaka kama inavyoelekezwa
na Tamko la Serikali no 306 la Septemba 1954 ambalo lilianzisha rasmi
msitu huo wa hifadhi kwa ajili ya kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji
kwa wakazi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani na vizazi vijavyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu akipitia ramani ya eneo hilo la Msitu wa Kazimzumbwi.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Lazaro Nyalandu akipatiwa maelezo na
Mmoja wa viongozi wa Wilaya ya Kisarawe juu ya Msitu wa Kazimzumbwi.
Nyalandu akizungungumza na Waandishi wa habari alioambatana nao.