Samahani kwa picha hizi
Mwananchuo
wa chuo cha ualimu cha ST Aggrey kilichopo uyole jijini mbeya
anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira
kali katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma zakuiba pikipiki zakusafirishia
abiria maarufu kama bodaboda.
Samahani kwa picha hizi
Hii ndiyo pikipiki inayodaiwa mwanachuo huyo kuiiba |
Hiki ni kitambulisho cha mwana chuo huyo |
Mgonja amesema tukio hilo limetokea mnamo july 2 mwaka huu majira ya saa 8 za mchana katika daraja lilopo karibu na hotel ya Rift Valley barabara yakuelekea isanga jijini mbeya.
Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada yakupewa taarifa za kuibiwa kwa pikipiki yenye No T 438BZU aina T-BETTER yenye alama ya chama cha Demokrasia na maendeleo mali ya JOSEPH KAPASI(23)mkazi wa Ilomba jijini hapa
Kwaupande
wake mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema aliombwa
kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae alipoanza kuendesha vizuri
alitokomea nayo na marabaada ya hapo alipatikana eneo la isanga
akielekea barabara ya chunya ili aibe na ndipo akakamatwa na wanainchi
wenye hasira kali nakuanza kumpa kichapo ambacho kimemfanya azirai.