Rapper na mtetezi wa haki za watu wenye ulimevu wa ngozi, mwanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Afrobino, Babu Sikare aka Albino Fulani, jana amegundua kuwa kuna biashara nzuri ukiwaangunisha Fid Q na MwanaFA kwenye ziara ya pamoja kipindi hiki.
Albino Fulani ameligundua hilo baada ya kuona jinsi wimbo wa MwanaFA aliomshirikisha AY na Dully Sykes uliyotoka mwezi uliopita ‘Ameen’ na wimbo wa Fid Q akiwa na Yvonne Mwale, ‘Sihitaji Marafiki’ zinavyojadiliwa na watu kwa utunzi wake.
Ni kweli kutokana na utunzi uliotukuka wa nyimbo hizo za manguli hao wa hip hop nchini, mashabiki wao wamekuwa wakiandika baadhi ya mashairi ya nyimbo hizo kwenye Twitter na Facebook na kuwapongeza kwa kufikiria mbali.
Uzuri zaidi mjadala huo kuhusu nyimbo hizo unaendelea hadi leo na watu hawachoki kuwapongeza.


“Soo happy to see that the most talked about musicians at this moment ni watu wangu wa karibu,Fid Q and MwanaFA #Honored Niandae #Tour4Two?” Albino Fulani alitweet jana.
Kwa upande wake wa Fid alijibu kwa kusema: Good idea.. Huku #KeepTheGoodMusicAlive kule *bring the #DarkWarriorMusic.
Naye MwanaFa alikubaliana na idea hiyo kwa kujibu, “Hahaha… ni food for thought my brodda!!”
Kama kweli kukiwepo tour ya nchi nzima ya wasanii hawa wawili wanaoheshimika kwa uandishi bora wa mashairi ya hip hop nchini, basi tutaifananisha tour hiyo na ile inayoendelea sasa barani Ulaya ya ‘Watch The Throne’ ya Jay-Z na Kanye West.
Swali tour yao itaitwaje? Keep the Good Music Aive Tour, Dark Warrior Music Tour ama Mwanza Meets Tanga Tour? Any suggestions!!!
This will be a sellout tour, no doubt about that. Think fast guys and go get that money!