Ukiniamsha usingizini ukaniambia nikutajie majina 5 ya wasanii wa sanaa ya maigizo nchini Tanzania,nina uhakika kabisa kwamba miongoni mwa majina hayo bila shaka nitakutajia Muhogo Mchungu.
Ni muigizaji mkongwe
katika sanaa na ambaye naamini endapo waigizaji wanaochipukia
wangechukua muda wao kutaka kujifunza kutoka kwake,basi wangefaidika na
mengi sana.
Ninachokipenda zaidi ni jinsi anavyoweza kuuvaa uhusika
katika namna ambayo ni halisi(natural acting).Ukimtazama unaona uhalisia
wa maisha na kile anachokiigiza.Naam,huo ndio uigizaji.
Lakini ungeniuliza jina lake,ningebaki kama Bubu.Macho yangenitoka na
akili kunizunguka.Nisingelijua.Ninalolijua mimi ni jina lake la
kisanii…Muhogo Mchungu.
Lakini alipofika pale Amaya Beauty Salon &
Spa na kuketi na Salama Jabir na wenzake John na Muba,aliulizwa jina
lake.Amelitaja zaidi ya mara moja.Ajabu,ninapoandika hapa bado nakumbuka
majina mawili tu ya mwanzoni yaani Abdallah Said…mengine je?
Yawezekana
nawe ukawa kama mimi kwamba hukuwahi kulijua jina lake halisi.
Msikilize
hapa Mhogo Mchungu akiongelea mengi.Alah..kumbe yeye na wale watoto wa
Jangwani ni..
Thankx, Celebraty bongo
MSIKILIZE MUHOGO MCHUNGU