Daudi Jairo(kushoto), akimkabidhi darubini ofisa elimu Mkoa Singida Yusufu Kipengere, kwa ajili ya shule sekondari Mwenge.
Na: Elisante John
Na: Elisante John
KAMPUNI
ya uuzaji vitabu G.B.S Ltd, ya Dar es Salaam, imetoa msaada wa darubini
tatu zenye thamani ya Sh.825,000 Mkoani Singida kwa ajili ya shule ya
tatu za Sekondari.
Shule zilizonufaika na msaada huo ni Mwenge (Iliyopo Manispaa Singida), Lulumba na Gumanga (Iramba.
Msaada huo umekabidhiwa na Meneja Kampuni ya G.B.S.Ltd kupitia ofisi zake zilizopo kanda ya kati(Dodoma), Daudi Jairo.
Jairo
amesema, licha msaada huo kuwa na lengo la kuongeza ufaulu kwa
wanafunzi wa masomo ya sayansi, pia ni kuhakikisha mwanafunzi wa kwanza
nchini anatokea Mkoa Singida.
Alisema
kuanzia mwaka 2009 hadi sasa kampuni hiyo imetoa msaada wa vifaa mbali
mbali vya kujifunzia shule za Sekondari, wenye thamani zaidi ya
Sh.Milioni tisa Mkoani Singida.
Kila darubini iliyotolewa msaada ina thamani ya Sh. 275,000.
Akipokea
darubini hizo kabla ya kukabidhi kwa walengwa, afisa elimu Mkoa Singida
Yusufu Kipengere alisema kuwa, Mkoa huo una jumla ya Sekondari 153,
lakini ni shule saba tu ndizo zenye maabara za kufanyia mtihani.