VYANZO VYA KUAMINIKA: BI KIDUDE BADO YUKO HAI

Asubuhi ya leo kumezagaa taarifa kuwa mwanamuziki mkongwe wa Taarab wa  Zanzibar, Bi. Kidude amefariki dunia. Radio ya Zenji FM ya visiwani humo nayo ilitangaza kifo chake. Lakini kutokana na vyanzo mbalimbali vya uhakika akiwemo mjukuu wake, Bi. Kidude bado yupo hai.
Mo Blog: Habari zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii kuwa mkongwe wa muziki wa jadi visiwani Zanzibar Bi. Kidude amefariki dunia si za kweli MO BLOG imezungumza na watu wa karibu ambao wamesema kwamba Bi. Kidude bado anavuta pumzi na amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal iliyopo visiwani humo.
Jamani habari kutoka chanzo cha uhakika zinasema Bi Kidude hajafariki yupo mahututi tu. Samahani wote niliowapotosha kwa tweet yangu.
— Uncle Fafi(@Tanganyikan) September 1, 2012
#BiKidude is not dead. According to mjukuu wake.
— Masanja Mkandamizaji (@mkandamizaji) September 1, 2012
Asubuhi hii Kuna habari mbaya zinasambazwa kuhusu mwimbajiMaarufu wa muziki wa taarabu Bi Kidude... Habari hizo ... m.tmi.me/wk53w
— Lameck Ditto (@Lameckditto) September 1, 2012
Hii si mara ya kwanza kwa Bi. Kidude kuzushiwa kuwa amefariki dunia.