SHEVCHENKO AAMUA KUKIMBILIA KWENYE SIASA.
|
Andriy Shevchenko. |
MSHAMBULIAJI wa zamani wa
Chelsea Andriy Shevchenko ametangaza kustaafu kucheza soka rasmi ili
aweze kujishughulisha na nmasuala ya siasa. Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Ukraine mwenye miaka 35 alithibisha taarifa hizo
ambazo zilitolewa katika mtandao wa klabu ya Dynamo Kiev ambayo alikuwa
akicheza. Shevchenko
amecheza mechi 111 kwa nchi yake ambapo mara ya mwisho ilikuwa katika
michuano ya Ulaya iliyomalizika mapema mwezi huu ambapo Ukraine
ilifungwa bao 1-0 na Uingereza. Mshambuliaji
huyo aliibukia katika klabu ya Dynamo mwaka 1994 na baadae kuhamia
klabu ya AC Milan mwaka 1999 ambapo alifanikiwa kushinda taji la Ligi ya
mabingwa ya Ulaya mwaka 2003 na klabu hiyo huku yeye akiwa ndio nyota
wa mchezo baada ya kushinda penati ya mwisho. Akiwa
na miaka 29 Shevchenko alihamia katika klabu ya Chelsea ambayo ilikuwa
ikifundishwa na Jose Mourinho mwaka 2006 kwa ada paundi milioni 30
lakini hakupata mafanikio katika misimu miwili aliyochezea klabu hiyo na
kuamua kurejea AC Milan ambapo nako hakukaa sana kabla ya kuamua
kurejea Dynamo mwaka 2009. Shevchenko
amefunga mabao 48 na kurekodi ya mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi
katika timu ya taifa ya nchi hiyo huku akikiongoza kikosi cha nchi hiyo
kilichofika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka
2006 na pia aliwahi kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya mwaka
2004.