Mkurugenzi wa Global Publishers, Erick Shigongo
MKURUGENZI
wa Global Publishers, Erick Shigongo amewataka Wasanii kuacha tofauti
zao katika kutetea maslahi ya nchi na si vinginevyo.
Kauli
hiyo ilitolewa jana, na Mkurugenzi huyo alipokuwa akizungumza na
wandishi wa habari kuhusu kuzulumiwa dola 3500 na msanii wa Uganda Jose
Chameleone.
Alisema
ameshangazwa na baadhi ya Watanzania kumchafua kwenye mitandao kwa
kitendo chake cha kumdai msanii huyo wa Uganda, fedha walizokubaliana
katika mkataba ili kufanya onyesho la Tamasha la Usiku wa Matumaini.
Shigongo
alisema huu ni wakati kwa watanzania kufahamu ukweli kuhusu hilo
kutokana na ukweli kwamba msanii huyo, amekiuka makubaliano ya mkataba
wa kwanza ambao walikubaliana kufanya onyesho hilo ghafla akageuka kudai
fedha zaidi.
Alisema
hata hivyo, Mkurugenzi huyo alikubali kuingia mkataba mwingine kwa mara
ya pili kutokana na ukweli kwamba alikwishafanya matngazo kuwa msanii
huyo angekua mmoja wa wasanii ambao wangefanya onyesho katika tamasha
hilo.
“Kweli
tulikubaliana mkataba mwingine nikamlipa dola 8000 na kweli alikuja
akafanya onyesho lakini baada ya hapo ndipo nilipomdai fedha zangu dola
3500 alizochukua katika makubaliano ya awali”alisema Shigongo.
Shigongo
alisema si kweli kwamba alizuia pasipoti ya msanii huyo wakati
alipokuwa amepangisha chumba kwenye hoteli yake bali kilichotokea ni
msanii huyo kuondoka mwenyewe baada ya kudaiwa fedha hizo.
Katika
hatua nyingine, Shigongo alisikitishwa na kitendo cha msanii huyo
akishirikiana na vijana wenzake kuvamia ubalozi wa Tanzania nchini
Uganda kwa madai ya kudai kurudishiwa pasipoti yake.