Wakazi wa Jiji Tanga wakuwa wamefurika kwa wingi kwenye Viwanja vya Tangamano kushuhudia burudani Mbali mbali zinazoonyeshwa kwenye Tamasha la Wazi la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) lenye udhamini Mnono kwa Kinywaji cha Grand Malt.
Ngoma Baikoko ndio iliyolinogesha Tamasha hili kwa linaloendelea kwa siku ya pili sasa katika viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga.
Watoto wa Jiji la Tanga wakionyesha umahiri wao wa kukisakata Kiduku mbele ya Watazamaji Lukuki waliofika kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga kufuatilia Tamasha la Wazi la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) ambalo linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Kinywaji chake cha Grand Malt.
Vijana wa IceCream Dancers wakionyesha mambo yao.
Mshereheshaji wa Tamasha hilo,Said mwana wa Kariakoo akifurahi na mmoja wa watoto waliopanda stejini na kuonyesha umahiri wake wa kusakata kiduku.
Tangamano mambo yalikuwa bam bam pale ulipofika kuda wa kucheki fainali za mataifa ya ulaya,maana mambo yalienda live bila chenga na kila mmoja alisuuzika na roho yake katika Tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sofia Productions na Mratibu wa Tamasha hilo,Mussa Kisoky (pili kushoto) akifuatilia tamasha hilo kwa makini.
wazee wa kazi mzigoni.