Bob Junior asusiwa Jukwaa Na Mke Mtarajiwa Kisa Mashabiki Wa Kike

Bob, G-Lover na mke wa Bob Msanii Bob junior ambaye anajulikana zaidi kama Sharobaro president ama Rais wa wasafi jana usiku aliweza kukonga Nyoyo za mashabiki kwa shoo ya nguvu katika ukumbi disco wa club Billicanas katikati ya jiji la Dar-Es-Salaam, usiku wa jana.
Msanii huyo alipanda stejini majira ya saa tisa kasoro usiku na moja kwa moja alilishambulia jukwaa kwa mbwembwe za hali ya juu huku akiongozwa na madansa wake wasafi classic crew. Bob Junior aliimba nyimbo tatu ikiwemo nyimbo ya ‘Na nini’, ‘oyoyo’ na his latest Mega hit ‘Nichum’.
Aidha katika shoo hiyo jambo moja tu ambalo lilikuwa linasubiriwa na watu wengi halikufanyika. Kutambulishwa kwa Yule kipenzi cha Bob Junior ambaye kwa wiki nzima matangazo pamoja na Bob Junior mwenyewe alikuwa akithibitisha kuwa atamtambulisha kwa jamii kwenye jukwaa hilo.
Inasemekana mpenzi wake huyo ambaye jana mchana familia ya Bob junior walikuwa wametoka kupeleka posa, alikasirika kwa kitendo cha Bob Junior kufuatwa jukwaani na mashabiki wake wengi wa kike ambao walimtunza pesa pamoja na kucheza nae, na wengine walidiriki Kumchumu ki ukweli kweli kuonyesha hisia zao za kishabiki kwake.
Kuona hivyo ‘Mamaa’ mtarajiwa alikasirika na kugoma kupanda stejini kwa ajili ya kutambulishwa, kwani ilibidi apande wakati wa wimbo huo wa Nichum, kama ambavyo Bob junior aliahidi.
Nyuma ya pazia inasemekana mtarajiwa wake alienda Backstage na kulalamikia kitendo hicho kwa Bob junior ikiwemo Kumsusia kuwa nae na kisha kuondoka ukumbini.
Huku yote hayo yakitokea Bob junior hakuonekana kupaniki na alibaki klabu na vijana wake wa wasafi classic pamoja na washkaji zake mpaka mida ya saa kumi ambapo ndipo alisepa.