DORIS MALIYAGA
DUME la mabao la Yanga, Said Bahanuzi anatarajia kutua leo Jumamosi
jijini Dar es Salaam akitokea kwao Mwanza alikokwenda kusaka baraka
baada ya kupapotea kwa miaka mingi.
Bahanuzi, ambaye nyota yake imeng'ara baada ya kutua kukitumikia
kikosi cha Jangwani chini ya kocha Tom Saintfiet kwenye michuano ya
Kombe la Kagame akitokea Mtibwa Sugar.
Ameliambia Mwanaspoti kuwa:"Nimeamua kufanya hivyo kwa sababu ni
kipindi kirefu, niliasi nyumbani, nikaona nifanye hivyo baada ya kupata
nafasi hii kwetu ni Sengerema, Mwanza."
Akizungumzia furaha yake baada ya kukamilisha ndoto zake za kuitwa
Taifa Stars, Bahanuzi alisema: "Nilitamani kwa kipindi kirefu kucheza
Taifa Stars hatimaye ndoto zangu zimefanikiwa. Nataka k