KONGAMANO LA HAMASA YA KUFUFUA TIMU YA TUKUYU STAR LAFANA UWANJA WA TANDALE MJINI TUKUYU

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh. Crispin Meela akizungumza na Mashabiki, Wadau na Wananchi wa Rungwe wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kuifufua timu ya Tukuyu Star kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu mkoani Mbeya leo, ambapo kulikuwa na michezo mbalimbali ya mpira wa miguu ikishereheswa na ngoma za asili ya watu wa Rungwe ya Ighoma iliyokuwa ikutumbuizwa katika viwanja hivyo, Bonanza lilivuta hisia za watu wengi na wadau wa mkoa wa mbeya na mikoa ya jirani hasa wachezaji waliowahi kuchezea timu ya Tukuyu Star miaka ya 1980 na 1986 huku umati wa watu ukishuhudia tukio hilo. Katika bonanza hilo timu ya Rungwe Veterani imefaikiwa kkuichapa timu ya wadau wa Tukuyu Star Family magolo 3-1, akielezea mpambano huo Kocha wa timu ya Tukuyu Star Family Kenny6 Mwaisabula amesema kushindwa ni sehemu ya mchezo, lakini pia wachezaji wa Rungwe Veterani wako fiti zaidi kimchezo kutokana na kwamba muda mwingi wanafanya mazoezi sana, lakini pia hali ya hewa inawaruhusu kwani wamezoea baridi tofauti na wachezaji wake, Usiku huu kuna kongamano linaendelea mjini Tukuyu ili kujadili mikakati mbalimbali na utaratibu utakaotumika katika kuiendesha Tukuyu Star mpya.
Makamu mwenyekiti wa Tukuyu Stars Family Bw. Peter Mwambuja akizungumza katika bonanza la michezo kwa ajili ya kuhamasisha wadau ili kufufua upya timu ya Tukuyu Star kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu leo
Kikosi kizima cha Tukuyu Star Family kikiwa katika picha ya pamoja kulia ni kocha Kenny Mwaisabula Mzazi na kushoto ni Makamu mwenyekiti Tukuyu star Family Peter Mwabuja.
Kikosi cha Tukuyu Star Family na Rungwe Veterani vikiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao kabla ya kuanza kwa mchezo wao.
Kocha Koroso naye alikuwepo katika bonanza hilo , Koroso ni mmoja wa makocha waliofundisha mpira nchini Tanzania na nje ya nchi.
Dasi wa Wilaya ya Rungwe Mosess Mwidete akikagua kikosi cha timu ya Rungwe Veterani kabla ya mchezo kati yake na Tukuyu Star Family.
Kikosi cha Tukuyu Star Family kutoka jijini Dar es salaam kikiwa katika picha ya pamoja na kochwa wao pamoja na viongozi kadhaa wa timu hiyo mbele ya gari lao
Mosess Mwidete DAS wa Wilaya ya Rungwe akizungumza na wachezaji wa Tukuyu Star Family na Rungwe Veterani kabla ya mchezo wao kwenyew uwanja wa Tandale mjini Tukuyu.
Kikosi cha timu ya Rungwe Veterani kikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu.
Wadau wa Tukuyu  Star Family  wakijadiliana jambo katika kongamano hilo huku wakishuhudia mpambano wao kati yao na Tukuyu Star Family.
Kocha Kenny Mwaisabula Mzazi akitoa maelekezo kwa wachezaji wake kushoto ni Moses Mkandawile na katikati ni Willy Martin "Gari kubwa"
Mashabiki mbalimbal;i wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Tandale ili kushuhudia Kongamano hilo.
Ngoma ya Asili ya kinyakyusa inayoitwa Ighoma ikitumbuizwa katika bonanza hilo kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali ya mpira wa miguu.
Timu ya U14 ya Ushirika mjini Tukuyu ikiwa katika picha ya pamoja
Timu ya U14  FOYSA kutoka jijini Mbeya kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kucheza mchezo wake na Ushirika
Mchezaji wa timu ya FOYSA akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Ushirika wakati timu za U14 zilipopambana katika bonanza hilo
Ngoma ya asili ya Kinyakyusa ikitumuiza katika bonanza hilo
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh. Crispin Meela wa pili kutoka kulia akizungumza mjambo na Mwenyekiti wa kamati ya Kufufua timu ya Tukuyu Star Kenny Mwaisabula, kulia ni Mosess Mwidete RAS wa Rungwe na kushoto ni Peter Mwambuja Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo
Mashabiki na wadau wa Tukuyu Star wakishuhudia michezo mbalimbali katika bonanza hilo.