CHADEMA leo yaingia Ulanga Kuendelea NaOperation Sangara


Operation Sangara pamoja na vuguvugu la mabadiliko leo imeingia Ulanga Mashariki ikitokea Kilombero. Mikutano imefanyika kwenye Kata 8 na Vijiji zaidi ya 24. Kesho itakuwa ni Kata 8 za Ulanga Magharibi na keshokutwa itakuwa ni Kata 4 za Mashariki na 4 za Magharibi. 
Ikikumbukwe Operation ni kwa ajili ya kujenga mtandao wa CHADEMA vijijini na kwenye vitongoji. Hivyo pamoja na Mikutano pia kumekuwa kukifanyika uchaguzi wa Chama kuanzia Vitongoji hadi ngazi ya Kata. Mh. Mponda amelazimika kurudi Jimboni ghafla baada ya kuwasahau Wananchi wake kwa muda mrefu.