KAHABA ATOA KICHAPO KIKALI KWA MLEMAVU ALIYE MDHULUMU 60,0000 AMBAYO ILIKUWA NI MALIPO YA USIKU MMOJA


VURUGU zilizuka nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro kufuatia kahaba mmoja kumchapa makofi mlemavu wa miguu,  Godlack Schone, 33, akimdai shilingi elfu 60 za ‘malipo’ ya huduma ya mapenzi aliyompa kwa usiku kucha.

Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita mjini Morogoro  na kuwalazimisha baadhi ya wafanyakazi wa mjengo huo kumjia juu changudoa huyo kwa kitendo cha kumpiga mlemavu mbele ya kadamnasi.

Akisimulia tukio hilo, karani mmoja wa ofisi hiyo anayefanya kazi upande wa utawala alisema chanzo cha ugomvi huo ni kahaba huyo kudai ‘haki’ yake baada ya kumpa ‘huduma’ ya mahaba Schone.

 Kufuatia tukio hilo kubainika, hakuna mtu aliyekuwa tayari kumsaidia tena mlemavu huyo, hivyo alilala nje ya ofisi hiyo hadi siku iliyofuata ambapo alikwenda kwenye Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Aziz Abood na kuomba msaada mwingine wa kurejeswa kwao ambapo alisaidiwa.