CHAMA cha waandishi wa habari mkoa wa Dodoma (CPC)wamelaani vurugu
zilizotokea juzi mkoani Iringa na kusababisha kifo cha mwandishi wa
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa chama hicho Habel Chidawali
alipokuwa akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari mkoani hapa.
Chidawali amesema kuwa kamwe chama hicho hakikubaliani na nguvu kubwa
iliyotumiwa na jeshi la polisi kwa ajili ya kumwaga damu ya mwandishi
huyo ambaye hakuwa na hatia na kamwe jeshi la polisi haliwezi
kujitetea kwa kudai kifo cha mwandishi huyo ni bahati mbaya.
Amesema kuwa
jeshi la polisi limekuwa likionyesha wazi wazi kuwa
linatumia nguvu,ubabe na matumizi mabovu ya silaha za moto ambayo
hayajaweza kusaidia siku zote na badala yake kinachoachwa ni maumivu
na vilio kwa wananchi.
Katibu huyo amesema kama jeshi la polisi linatuliza ghasia hakuna
siku hata moja haijatokea wakamuua kiongozi yoyote wa siasa ambao ni
vinara wa mikutano mbalimbali.
Kwa upande wao wananchi mbalimbali mkoani hapa wamekemea nguvu kubwa
inayotumika na Polisi katika vurugu mbalimbali zinazotokea.
Wamesema tabia ya jeshi la polisi kutumia nguvu na silaha za moto
ambazo zinasababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia.
Catheline Muhinte, amesema kuwa tukio lililofanywa na jeshi la polisi
la kumuua mwandishi wa habari linaonyesha dhairi kuwa kwa sasa jeshi
hilo linafanya kazi kwa kukiuka maadili ya malengo yao.
Amesema katika mwonekano wa picha ambazo zinaonekana katika vyombo
mbalimbali vya habari
inaonyesha dhairi kuwa polisi walihusika moja
kwa moja na kifo cha mwandishi huyo.