Z-ANTO APATA SHAVU LA KUPIGA SHOW YA MWAKA NCHINI ZAMBIA MBELE YA RAIS
Msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo, hitmaker wa ngoma ya ‘Kisiwa cha Malavidavi’, Z-anto, ameumbia mtandao huu
kuwa amepata mualiko mkubwa Wa Serikali ya Zambia kwenda kupiga show
nchini humo Septemba 24 mwaka huu huku mgeni rasmi akiwa ni rais wa
nchini hiyo .Msanii huyo alisema kuwa nchi hiyo huwa inasherekea sikukuu yao kila
mwaka ingawa hajajua ni sikukuu ya aina gani ingawa kwa taarifa
aliyopata ni kuwa siku hiyo wazambia wote huwa hawaendi kazini.
Alisema sasa yupo katika maandalizi ya ishu hiyo ili aweze kuwawakilisha
hata wasanii wengine wa Tanzania kwani anaamini safari hiyo haitakuwa
ya pekee yake kwani nyuma yake atalibeba taifa la Tanzania.
“Yani ishu ambayo inanisumbua kichwa hapa ni juu ya maandalizi yangu
ya safari ya kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya kupiga show ambayo
mwaliko wake ni mkubwa sana hiyo nawaomba watanzania waniombee niweze
kujiandaa vizuri,” alisema.