
Maadhimisho
ya Wiki ya Nenda kwa Usalkama barabarani leo yameingia siku ya Pili
ambapo kitaifa yanafanyika mjini Iringa katika Uwanja wa Sokoine na
kushirikisha wadau mbalimbali wa Usalama barabarani. Kauli mbiu ya
Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO,
ZINGATIA SHERIA”. Pichani ni Meneja Masoko na Utafiti wa Shirika la
Bima la Taifa (NIC) akitoa maelekezo kwa vijana na watoto waliofika
bandani hapo leo.

Miongoni
mwa washiriki wa Maonesho ya mwaka huu ya wiki ya Nenda kwa Usalama ni
Kampuni ya ASAS ambao mbali na shughuli za usafirishaji wa mizigo pia ni
wazalishaji wakubwa wa Bidhaa za Maziwa ambayo asilimia kubwa
hupatikana kutoka katika mashamba ya mifugo ya ASAS DAIRY FARM yaliyopo
mkoani Iringa. Ng’ombe wa kisasa, Mbuzi, kondoo, Ngamia na Farasi ni
miongoni mwa mifugo inayofugwa katika mashamba hayo.
Pichani
ni baadhi ya wananchi wa mjini Iringa wakiwa katika banda la ASAS Dairy
Farm wakiangalia Ngombe, Farasasi, Nyati na Ngamia waliopo katika
maonesho hayo leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA
AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.

Wananchi
wa mjini Iringa wakiwa katika banda la ASAS Dairy Farm wakiangalia
Nyati (Mbogo Maji) waliopo katika maonesho hayo leo. Kauli mbiu ya
Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO,
ZINGATIA SHERIA”.

Watoto wa
mjini Iringa wakiwa katika banda la ASAS Dairy Farm wakiangalia Ngamia
waliopo katika maonesho hayo leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka
huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.

Wananchi
wa mjini Iringa wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa mmoja wa maofisa
wa TANROADS walipotembelea katika banda hilo lililopo pamoja na Wizara
ya Ujenzi. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI
ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.

Watu
mbalimbali wakiwa katika Banda la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)
wakiangalia gari maalum la kufundishia madereva lililopo bandani hapo.

Watoto
ndio umri sahihi kutoa mafunzo ya namna ya matumizi sahihi ya barabara.
Na iwapo kama watoto hawa watapata elimu ya kutosha juu ya utumiaji wa
barabara itachangia kwa kiwango kikubwa yatachangia kupunguza kiwango a
ajali za barabarani miaka ijayo. Hapa watoto wakimsikiliza ofisa wa
Wizara ya Ujenzi.

Wananchi
wa mjini Iringa wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa mmoja wa maofisa
wa Wizara ya Ujenzi walipotembelea katika banda hilo jana. Kauli mbiu
ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA
VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.

Wananchi
wa mjini Iringa wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa mmoja wa maofisa
wa Jeshi la Polisi walipotembelea katika banda hilo lililopo katika
viwanja vya Samora mjini Iringa yanapofanyika maonesho ya maadhimisho ya
wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka
huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.


Mara
nyingi zinapotokea ajali Hospitali huwajibika kwa kiwango kikubwa
kuhakikisha afya za watu zipo zinarejea katika hali ya kawaida na
kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa. Katika Maonesho ya mwaka huu
ya wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani kitaifa mjini Iringa, Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wanashiriki na hapa watu mbalimbali wakipata
ushauri na kuangaliwa afya zao. Nenda kwa Usalama kitaifa. Kauli mbiu ya
Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA
VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.