
Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Wenger amesema kuwa anamwamini Bould kwakuwa amekuwa akifanya kazi yake vyema na huko mbele atakuaja kuwa kocha mzuri kwasababu vigezo anavyo. UEFA ilimfungia Wenger baada ya kumkashifu mwamuzi Damir Skomina wakati wakielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya AC Milan msimu uliopita. Wenger anatakiwa kuitumikia adhabu hiyo ndani ya miezi 12 wakati michuano hiyo itakapokuwa ikiendelea.