Mama Tunu Pinda Azindua Maonyesho Ya Wanawake
Mke wa Waziri Mkuu Mana Tunu Pinda akitoa
hotuba ya kufungua Maonyesho ya Wanawake Wajasiriamali (MOWE) katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja jana jijini Dar es Salaam ambapo amewahimiza
wajasiriamali kujiunga katika ushirika ili iwe rahisi kusaidiwa kupata
mikopo, kutafuta masoko, kupanga bei nzuri ya bidhaa zetu, kupata
utaalam na teknolojia mpya. Kauli Mbiu ya ya Maonyesho hayo mwaka huu ni
“Msichana Amka, Ujasiriamali ni Ajira”.
Mama Tunu Pinda akikata utepe kuzindua Mradi
wa Uwezeshaji Kiuchumi wa Maendeleo ya Wanawake Wajasiriamali (WEDEE)
Ulio chini ya Shirika la Kazi Duniani (WEDEE) wakati wa ufunguzi wa
Maonyesho ya Wanawake wajasiriamali ya MOWE yanayoendelea katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja baada ya kufungua maonyesho ya MOWE 2012
Vibanda vya maonyesho