MDOMO WAMPONZA CHAZ BABA.......NI BAADA YA KUTANGAZA KUMUOA LULU MICHAEL NA MAMBO KWENDA KOMBO
RAIS
wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ yupo kwenye
gogoro zito na wanawake aliozaa nao, mama Jack na mama Carina baada ya
hivi karibuni kutangaza ndoa na staa wa filamu aliye gerezani, Elizabeth
Michael ‘Lulu’.
Akiongea na mwandishi wa habari hii, Chaz Baba
alisema katika stori za magazetini kwa mwaka huu, ya kumuoa Lulu
imemfikisha pabaya.
“Ilipotoka tu ile habari, wakanipigia simu kila
mmoja kwa wakati wake, maswali mengi, nilijaribu kuwaweka sawa lakini
hakuna aliyenisikiliza zaidi ya kunikatia simu,” alisema Chaz Baba.