Aslay: Nimezifahamu tuzo za Kora jana
Msanii wa hit ya Nakusemea, Aslay ambaye ametajwa kuwania katika tuzo
zenye thamani kubwa barani Afrika za Kora, Aslay, amesema alikuwa
hazifahamu tuzo hizo hadi jana.Akiongea kwa simu na Bongo5 Aslay
amesema alipoambiwa kwa mara ya kwanza hakuamini na baada ya kuambiwa
ukubwa wa tuzo hizo alikuwa na furaha isiyoelezeka.
“Mara ya kwanza ile nilikuwa sifahamu, nimezifahamu jana hiyo hiyo watu ndio wananiambia bwana tuzo kubwa sana hizo,” amesema.
“Najisikia vizuri kwasababu namshukuru mwenyezi Mungu kwanza kwa nilikotoka mpaka hapa nilipofika kwahiyo nina furaha tu.”
Aslay ametajwa kuwania kipengele cha msanii anayechupikia barani Afrika.