Aunty Lulu "Nguo za Ndani Zimeniharibia Makalio Yangu na kufanya yawe na Mabaka"
MSANII asiyeishiwa na matukio, Lulu Mathias ‘Aunt Lulu’ amefunguka
kwamba kuharibika kwa mwili wake hasa kwenye makalio kumetokana na kuvaa
nguo za ndani aina ya ‘bikini’ ambazo zimechimba mistari.
Akizungumzia tabia ya mastaa wengi kutokuvaa nguo za ndani wanapokuwa
kwenye mitoko, Aunty Lulu alisema kuwa, hiyo inatokana na jinsi
zinavyowaathiri sehemu zao ‘muhimu’ na kwamba yeye ni mmoja wa
waathirika.
“Kwa kweli hizi nguo za ndani hasa
bikini zinatuharibu sana hasa sisi tuliojaaliwa kuwa na maumbile
makubwa, nilikuwa navaa lakini kwa kweli zimenichimba sana kiasi cha
kuniharibu na kupoteza mvuto wangu, sivai tena…nitaangalia ustaarabu
mwingine,” alisema msanii huyo.