MSANII WA VICHEKESHO NA MUZKI SHARO MILIONEA AMEFARIKI LEO HUKO MUHEZA TANGA KWA AJALI YA GARI AMBAPO NDUGU YAKE WA KARIBU SNURA MUSHI AMETHIBITISHA TUKIO HILO KWA NJIA YA SIMU .....
Naye Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Afande Constatine Masawe, amethibitisha kutokea kwa kifo cha wa Sharobaro, kufuatia ajali ya gari katika kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga ambako ndio nyumbani kwao.......
MPAKA SASA MWILI UPO TEULE MUHEZA HOSPITAL,TANGA
Mpekuzi imepokea habari hizi kwa mstuko na masikitiko makubwa kwani
nyota ya Sharo Milionea ndiyo ilikuwa inaanza kung'ara katika anga za
muziki pamoja na matangazo ya biashara, akiwa kayapumulia pumzi mpya wa
ubunifu na weledi katika kupeleka ujumbe kwa watazamaji ambao wakubwa na
wadogo walimpenda.
Mola aiweke roho ya marehemu
mahali pema peponi - Amina