Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa Mufti wa
Zanzibar Sheikh Fadhili Soraga ambaye amelazwa katika chumba cha dharura
katika Hospitali ya Taifa ya Muhiombili kufuatia majeraha ya usoni na
kifuani yaliyotokana na kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana
wakati akifanya mazoezi katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe mjini Unguja
juzi
Rais ambaye amerejea leo Jumanne Novemba 6, 2012 akitokea katika
ziara ya kikazi ya takriban juma moja katika mikoa ya Kilimanjaro,
Arusha, Manyara na Singida, amemtakia Sheikh Soraga nafuu ya haraka.
PICHA NA IKULU