Kijana
mmoja aliyetambulika kwa jina la Henry amejikuta mikononi mwa vyombo
vya dola baada ya kumchoma mkewe sehemu mbalimbali za mwili kwa
kutumia pasi na kumuua mtoto wake wa mwaka mmoja kwa madai kuwa
mwanamke huyo amekuwa akitoka kmaenzi na baba yake mzazi........
Akiongea kwa majuto makali huku akiwa "nyuma ya nondo", Henry anadai kuwa alifanya hivyo bila kukusudia
"Nakiri kwamba nilifanya maamuzi
ambayo sikutegemea kuyafanya katika maisha yangu.Nilikuwa napandwa na
hasira kubwa kila nikimuona yule mtoto akiamka na kulilia maziwa .
Moyo
ulikuwa ukijaa nakunifanya nishindwe hata kupumua na ndipo siku moja
ndani ya moyo wangu nilisikia sauti ikiniamuru nimuue yule mtoto maana
si damu yangu.
Bila kujizuia, nilimshika shingoni, nikamkaba na kumpiga kwa nguvu......." Henry alielezea tukio hilo huku aimwaga machozi ya uchungu
"Najua kuanzia sasa maisha yangu
yatakuwa ni gerezani tu.Nakubaliana na yote ila nimeona ni bora
jamii iujue ukweli.......
Mke wangu Mercy alikuwa na mahusiano
ya kimapenzi na baba yangu mzazi .Kabla ya tukio hili, nimekuwa
nikimuonya mara nyingi sana kwamba aache tabia hiyo na asiende
nyumbani kwa baba maana nilikuwa nimeshausoma mchezo huo.Mbaya zaidi
mke wangu hakutaka kunisikiliza.....
Siku moja mke wangu aliaga kuwa
anataka kwenda kwa rafiki yake.Nilimkataza na kumwambia kuwa asitoke
wala kwenda kokote lakini hakunisikia.Baada ya muda kidogo nilizuga
na kumwambia kuwa natoka kidogo.Baada ya nusu saa nilirudi nyumbani na
sikumkuta mke wangu.....
....Nilisubiri kidogo huku akili
ikiwa haifanyi kazi.Baadaye moyo ulinituma kuwa niende kwa baba
nikamuangalie maana si mbali sana kutoka nyumbani........
Nilifika na
kugonga mlango.Baba alitoka akiwa amejifunga taulo tu.Nilipojaribu
kuingia ndani alinizuia.Baada ya kuzozana naye kwa muda niliamua
kuacha na kurudi nyumbani.......Sijui mke wangu alitorokaje na
kuniwahi kufika nyumbani, lakini niliporudi nilimkuta ameshafika.
Badala ya kuchukia, nilijiuta nacheka sana
.yaani nilikuwa kama mtu aliyerukwa na akili.Nilijisogeza pembeni na
kuanza kuvuta sigara ili kupunguza hasira......
Ilipofika usiku,
nilichukua nguo yamteja wangu na kuanza kuipiga pasihuku nikiwa na
mawazo mengi.Baadae nilisikia sauti ndani ya moyo wangu ikiniambia
nijikaze japo nimulize ili niujue ukweli.Wakati huo pasi ilikuwa ni ya
moto kwelikweli. Ghafla maamuzi yakaniijia kuwa niitumie ile pasi
kumtisha ili aniambie ukweli wa tukio zima......
Nilimsogelea na kumwamsha.Alipoamka nilimuomba
anieleze ukweli tena kwa nia nzuri kabisa.Mercy hakunijibu kitu na
badala yake alikaa kimya.Nilijawa na hasira na kujikuta namchoma
kwa kutumia ile pasi
Nilipofanya
vile,Mercy alikiri kuwa amewahi tembea na baba yangu mara
tatu.....Aliposema vile hasira zilinipanda zaidi na kujikuta namchoma
zaidi......
Wakati
nafanya vile,mtoto aliamka na kuanza kulia kama ishara ya kutaka
kunyonya.Nilimwangalia kwa hasira huku moyo ukiniambia kuwa yule si
mwanangu...."
Henry alikaa kimya kwa muda huku
akiwa amejiinamia.Baada ya muda kidogo alinyanyua kichwa na
kuangalia juu huku uso wake ukiwa umelowa machozi....
Baada ya kimya cha muda, Henry aliendelea kwa kusema kuwa:"Yalikuwa
ni maamuzi mabaya sana.Wakati yule mtoto akilia, nilimshika na
kumkaba shingo.Baada ya kumkaba nilimpiga kwa ngumi.