Rais Barack Obama ameshinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu
sana kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni Michigan na Pennsylvania,
pamoja na mengine ambayo alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2008.
Mwenzake wa Republican Mitt Romney
ameshinda katika majimbo mengine muhimu pia ya Republican pamoja na
kushinda Indiana ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka 2008.
Mamilioni ya watu walijitokeza kupiga kura siku
ya Jumanne. Mshindi huenda akajulikana baada ya masaa kadhaa kuanzia
sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu yakitolewa.
Kura za maoni kabla ya kufanyika uchaguzi huu
zilionyesha kinyang'anyiro kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi wa
kura chache tu Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza kufungwa mapema
katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya Virginia na Ohio
nayo yakifunga mapema.
Kwa sasa kura za Electoral College zinaonyesha Obama yuko nyuma ya Romney kwa kura sita