VIDEO YA RAH P AKISIMULIA JINSI ALIVYOTESWA NA KUZALISHWA WATOTO WAWILI NCHINI MAREKANI


Kwa muda mrefu rapper wa kike aliyewahi kutikisa nchini Tanzania, Rah P amekuwa kimya na kuendelea na maisha yake nchini Marekani. 
Lakini wengi hawajui tabu na shida alizozipata baada ya kwenda nchini humo kutafuta maisha na kufuata ndoto yake. Hii ni interview iliyofanywa na Kali TV Online ambapo anasimulia jinsi alivyohangaika baada ya kuzalishwa watoto wawili na mwanaume ambaye alikuja kugundua kuwa ni muuzaji wa madawa ya kulevya.

Baadaye mwanaume huyo alikuja kukamatwa na hivyo kubaki mwenyewe akiwahudumia watoto wake wakati hakuwa na kazi. Baada ya hali hiyo alijikuta katika wakati mgumu na kusongwa na mawazo mengi kiasi cha kumfanya awe mlevi na kujikuta akifungwa jela.
Sasa anataka kufufua tena ndoto yake ya kufanikiwa kimuziki nchini Marekani. Atafanikiwa akiwa tayari ni mama wa watoto wawili?