Baadhi
ya wahitimu wa chuo kikuu cha Dodoma wakiwa kwenye foleni tayari kwa
kuchukua majoho yao ambayo watayavaa katika sherehe za kumalizia safari
yao ya miaka mitatu ya masomo yao ya Chuo Kikuu Cha Dodoma hapo Jana na
leo
Foleni
ikiwa haisogei kabisa huku wengine wakiendelea kusubiri na wengine
kupiga stori mara baada ya kutokuonana takribani miezi minne tokea
walipomaliza masomo yao chuoni hapo
Wahitimu
wa Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na
Lugha wakiwa kwenye foleni ya kuchukua majoho tayari kwa kuhudhuria
sherehe za mahafali ya tatu ya chuo kikuu cha Dodoma
Hapo
mwenye nguvu ndie alikuwa wa kwanza kuingia na mnyonge alisubiri yote
hiyo wakigombania kuingia wa kwanza kwaajili ya kuchukua majoho tu
Huku
wengine wakiwa wamejikalia zao chini wakisubiri vurugu za kuingia
kwaajili ya kuchukua majoho ziishe nao waingie kuchukua majoho yao
Baadhi
ya wahitimu mara baada ya kuchukua majoho yao tayari kwaajili ya
sherehe za mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu cha Dodoma yanayonyika leo tarehe 21 na 22 novemba 2012 katika viwanja vya Chimwaga
Chuoni hapo
Mara
Baada ya Kuchukua Majoho yao Wahitimu hawa waliyajaribu kwanza kuona
yanawatosha huku wengine wakisema kuwa "safari hii Majoho Yanatolewa Kwa
GPA likikuenea GPA yako ni kubwa lisipokuenea GPA Yako ni Ndogo"