KALA JEREMIAH AJIANDAA KUACHIA ALBAM YAKE YA KWANZA " PASAKA"



Baaba ya maandalizi makubwa mkali Kala Jeremiah sasa ametangaza kuwa albam yake yenye nyimbo 23 ipo kwenye matayarisho ya mwisho. Albam yake itaitwa Pasaka ikiwa na maana ya ukombozi. Kama alivyowaahidi mashabiki wake mwisho wa mwezi huu albam hiyo itakuwa sokoni na itakuwa albam yake ya kwanza iliyotayarishwa kwa muda mrefu lakini atakuwa akiisambaza mwenyewe.

Amesema ikiingia sokoni atatoa maelekezo ya sehemu gani itakuwa inapatikana lakini pia atatoa namba za simu ambazo watu wataruhusiwa kupiga na kuongea nae moja kwa moja.
“Albam inakwenda kwa jina la “Pasaka” maana yake ni ukombozi,ndani ya albam hii kuna wimbo ambao unaitwa pasaka ambao umebeba jina la albam ambao ki ukweli ndo wimbo ambao mimi kama KALA JEREMIAH naupenda sana kutokana na ubunifu uliotumika katika wimbo huu,kiukweli wewe mwenyewe ukisikia utaogopa sana,sio wimbo wa kawaida lakini pia utapata kusikia ngoma mbalimbali za ki harakati,” anasema Kala kwenye maelezo yake.
Amesema katika albam hiyo kutakuwa na ngoma za mapenzi, ngoma za usaliti, maombi,na kadhalika na jumla ya mambo yote hayo ndipo alipopata neno pasaka, ambalo linatokana na mapenzi, mateso,maombi, na usaliti, na mwisho kutokana na albam kuwa na mambo mengi ikiwa ni ukombozi pia.