Katibu Mkuu wa Chadema, Dk WilIbrod Slaa (Kulia) akiwa na makada wa
chama hicho ambao majina yao hayakupatikana, wakiandaa taarifa kabla ya
kuanza kwa siku ya pili ya kikao cha Kamati Kuu jana, Dar es Salaam.
Picha na Venance Nestory
Na: Joseph Zablon na Mussa Juma,Arusha
MGOGORO mkubwa unakinyemelea Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), baada ya kuelezwa kuwa sekretarieti yake imekayakataa
mapendekezo ya Tume ndogo iliyoundwa kuchunguza kukwama kwa miradi mingi
ya maendeleo, ukiwamo wa Maji Karatu Vijijini (Kaviwatu), ambayo
ilitaka baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mradi huo wafukuzwe.
Mradi huo wa maji unaelezwa kusababisha mpasuko
mkubwa ndani ya chama hicho hasa baina ya sekeretarieti ambayo inadaiwa
kuwakingia kifua baadhi ya watuhumiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu
ya chama hicho ambao wanataka hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson
Mwigamba alisema kwamba baadhi ya viongozi wa Chadema Wilaya ya Karatu
uliko mradi huo walihojiwa jana, lakini akasema hapakuwa na mpango
wowote wa kufukuzana.
“Ninachoelewa ni kwamba waliitwa wakahojiwa na
kitakachofuata ni kupewa maagizo ambayo lazima wayafuate na atakayekiuka
ndiye atakayefukuzwa,” alisema Mwigamba.
Baadhi ya viongozi wa Chadema Karatu waliotarajiwa
kuhojiwa jana ili kupata suluhu ya mgogoro huo ni pamoja na Mbunge wa
Karatu, Mchungaji Israel Natse, Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Pareso
na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Karatu, Lazaro Maasai na Diwani
wa Karatu Mjini, Jubiless Mnyenye.
Viongozi wakuu wa Chadema hawakupatikana jana kwa
kuwa muda mwingi walikuwa katika kikao hicho ambacho kilimalizika jana,
huku ikielezwa kuwa taarifa rasmi kuhusu yaliyojadiliwa itatolewa leo.
Alipoulizwa kuhusu mgogoro huo, Msemaji wa Chadema
Tumaini Makene alisema agenda za kikao hicho zilikuwa wazi na
ziliainishwa katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi.
“Hakuna zaidi ya hizo na leo (jana), ni masuala ya Katiba Mpya. Kwenye yatonakayo, masuala mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya nchi yanajadiliwa nchi nzima kwa sababu yanatokana na vikao vilivyopita si Karatu pekee. Angalia usije ukalishwa matangopori,” alisema.

Kumshinikiza Rais
Habari zaidi kutoka katika kikao hicho zinaeleza kuwa kamati hiyo imeazimia kuchukua hatua ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kusimamia utekelezaji wa masuala ambayo yapo katika mamlaka yake ikiwa ni pamoja na kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.

Wengine ambao kimesema kinataka wawajibishwe ni
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Said Mwema, Mkuu wa
Operesheni wa Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Morogoro, Faustine Shilogile.
Kamati hiyo pia imeazimia kuanzia Januari kuwa na
operesheni kubwa ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), nchi nzima kushinikiza
utekelezaji hatua za kinidhamu kwa watendaji hao na watuhumiwa wa
ufisadi wa Fedha za Madeni ya Nje (Epa).